Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewataka wazee wa mkoa huo kuhamasisha jamii kujitokeza kupiga kura Oktoba 29, 2025, na kuhakikisha vijana wanalinda amani ya nchi.
Amesema wazee wanayo nafasi kubwa katika kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo, akibainisha kuwa Dodoma ya sasa imebadilika na kuwa mji wa kuvutia kutokana na jitihada za Serikali.
Aidha, Senyamule amesema Serikali inaendelea kutoa elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa ili kuimarisha afya za wazee.
Wazee hao wametumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuboresha huduma za afya na miundombinu, huku Mkuu wa Mkoa akiahidi kushughulikia changamoto hizo na kuhakikisha wazee wanapewa kipaumbele siku ya kupiga kura.
✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates