#HABARI: Mgombea mwenza nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Balozi Dokta Emmanuel Nchimbi ameendelea na kampeni zake wilayani Kibondo mkoani Kigoma akinadi sera na kutoa ahadi za chama hicho za kuwaletea maendeleo katika kipindi cha miaka mitano ijayo endapo wananchi wa wilaya hiyo watakichagua tena kushika dola.

Akiwa katika viwanja vya shule ya msingi Kibondo, Nchimbi kando na ahadi zingine za kuboresha huduma za kijamii amesema watakwenda kuimarisha diplomasia ya kiuchumi ambayo mpaka sasa mgombea nafasi ya urais kwa chama hicho Dokta Samia Suluhu Hassan ameifanya vizuri sana hasa kwa nchi zinazotuzunguka.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *