#HABARI: Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini, imekamata na kuteketeza dawa za kulevya aina ya mirungi, zenye uzito wa zaidi ya kilogramu 374.
Uteketezaji huo umefanyika katika dampo la Serikali la Mtakuja lililopo wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro, na umefanyika kwa kufuata taratibu zote za kisheria, ukiwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo vyombo vya ulinzi na usalama.
Akizungumza kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas James Lyimo, Mwanasheria wa Mamlaka hiyo Benson Mwaitenda, amesema mirungi hiyo ni sehemu ya dawa za kulevya zinazoendelea kukamatwa katika operesheni endelevu zinazotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Kwa mujibu wa Mwaitenda, baadhi ya watuhumiwa wamekwishakamatwa na hatua za kisheria zinaendelea, huku akiwataka wananchi wa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga kujiepusha na biashara haramu ya dawa za kulevya zikiwemo mirungi na bangi, kwani sheria inakataza vikali na adhabu ni kubwa ikiwemo kifungo cha maisha pamoja na kutaifishwa kwa mali zinazohusishwa na biashara hiyo kama nyumba na vyombo vya usafiri.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania