#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa watumiaji wa maji kwa shughuli za kilimo katika maeneo ya kingo za Mto Ruvu, kusitisha matumizi ya maji hayo kwa muda, hadi mvua zitakapoanza kunyesha kwa wingi.
Wito huo umetolewa wakati Mkuu huyo wa Mkoa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua na kutembelea mitambo ya uzalishaji maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu.
Kunenge amesema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha kupungua kwa kasi kwa kiwango cha maji, hususan katika eneo la Ruvu Chini, kutokana na shughuli nyingi za kibinadamu kwenye mto huo.
“Tunafahamu kuwa watumiaji wa maji ni wengi na wengi wana vibali. Hivyo nawaomba watumiaji wote wawe wavumilivu katika kipindi hiki hadi mvua zitakapoanza,” amesema Kunenge.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania