#HABARI: Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Kampuni ya Africa Global Logistics (AGL) Tanzania Ltd, kampuni tanzu ya MSC yenye makao yake nchini Ufaransa, kwa ajili ya usanifu, ujenzi na uendeshaji wa gati tatu za kisasa katika Bandari ya Bagamoyo.
Hati hiyo imesainiwa katika Makao Makuu ya TPA jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Plasduce Mbossa, pamoja na Rais wa AGL, Bw. Philippe Labonne.
Akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano hayo, Bw. Mbossa amesema hatua hiyo ni ishara ya utayari wa kuanza rasmi mradi wa Bandari mpya ya Bagamoyo, na kubainisha kwamba katika awamu ya kwanza, AGL itaanza kazi za usanifu na ujenzi wa gati tatu kati ya jumla ya gati 28 zitakazojengwa katika bandari hiyo, pamoja na ujenzi wa gati mbili mpya za kisasa katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Bw. Labonne amesema AGL imeamua kuwekeza nchini Tanzania kutokana na mazingira mazuri ya amani, usalama na utulivu wa uwekezaji, pamoja na nafasi ya kipekee ya kijiografia ambayo Tanzania inayo katika sekta ya usafirishaji na biashara, na Tanzania ni lango muhimu la biashara Kitaifa na Kimataifa, hivyo kuifanya kuwa eneo lenye mvuto mkubwa wa uwekezaji.
Mradi wa ujenzi wa gati hizo tatu mpya katika Bandari ya Bagamoyo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 36 (Miaka itatu), AGL imepata nafasi ya kushirikiana na TPA katika mradi huu kutokana na uzoefu wake mkubwa katika kutoa huduma za usafirishaji na usimamizi wa mizigo, pamoja na huduma kamili za kimataifa za usafirishaji, forodha na Lojistiki.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.