#HABARI: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Mhe.Joel Nanauka, amewasihi vijana katika ngazi ya vyuo vikuu nchini, kutumia mijadala na masomo ili kuwa na uwezo wa kujenga hoja na fikra chanya za kukuza maendeleo ya Taifa na uzalendo.

Mhe. Nanauka amesema kuwa zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania ni vijana chini ya miaka 35 na hivyo kuhitaji kujumuishwa kwenye mipango ya maendeleo.

Waziri Nanauka amesema hayo wakati alipokutana na kuzungumza na Vijana wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Jijini Dar es Salaam.

Waziri Nanauka amewaeleza vijana hao dhamira ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzisha wizara maalum inayoshughulikia Maendeleo ya vijana nchini na kwaba serikali imeendelea kuimarisha sera, programu na fursa zinazowawezesha vijana kupata elimu bora, ajira, ujuzi, mitaji, huduma za afya pamoja na mazingira rafiki ya ushiriki katika shughuli za kijamii, kiuchumi na Kisiasa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *