Wizara ya Afya ya Gaza imetangaza kuwa, ukosefu wa dawa na vifaa vya matibabu huko Gaza unaongeza zaidi maafa ya kibinadamu katika eneo hilo.

Wizara ya Afya ya Gaza imetoa taarifa inayoashiria ukosefu wa dawa na vifaa vya matibabu huko Gaza, na kusisitiza kuwa asilimia 52 ya orodha ya dawa muhimu, asilimia 71 ya orodha ya bidhaa za matibabu, na asilimia 70 ya vifaa vya maabara havipo kabisa huko Gaza.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mzozo wa Gaza unazidi kuongezeka huku kukiwa na hitajio kubwa la kuingilia matibabu kwa waliojeruhiwa na wagonjwa.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa, huduma za msingi, upasuaji, wagonjwa mahututi, saratani na magonjwa ya damu ni miongoni mwa huduma zinazokabiliwa na uhaba mkubwa katika orodha ya dawa. Upasuaji wa mifupa, figo na dayalisisi, macho, upasuaji wa jumla, idara za upasuaji na wagonjwa mahututi pia zinakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na uhaba wa vifaa vya matibabu.

Katika taarifa hiyo, Wizara ya Afya ya Gaza ilitoa wito wa kuimarishwa mara moja kwa msaada wa matibabu ili kuwawezesha wafanyakazi wa matibabu katika idara maalumu.

Licha ya kusitishwa mapigano huko Gaza, lakini bado mateso ya njaa na ukosefu wa usalama na utulivu wa nafsi yanaendelea kuzisumbua familia za Wapalestina. Foleni ndefu za watu wenye njaa wanaosubiri kupata angalau mlo mmoja kwa siku zinaendelea kuonekana katika pembe mbalimbali za ukanda huo huku jeshi katili la Israeli likiendeleza mashambulizi ya mara kwa mara na kuzuia kuwafikia misaada wananchi hao wasio na ulinzi.

Ripoti kutoka Gaza zinaonyesha kuwa, mistari mirefu inaonekana kila siku kwenye vituo vya kugawa chakula cha hisani kwa matumaini ya kupokea angalau mlo mmoja kwa siku, huku jeshi la Israel likiendelea kuzuia malori ya misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *