
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco leo JUmatatu imetangaza kuwa mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa yamesababisha vifo vya takriban watu 37 katika mji wa pwani wa Safi nchini humo.
Mamlaka husika za Morocco zimearifu kuwa mvua mkubwa iliyonyesha usiku kucha na kusababisha mafuriko imesomba takriban nyumba 70, kuharibu biashara na kusomba magari 10.
Wakati huo huo,ripoti zinasema kuwa skuli zimetangaza kufungwa kwa muda wa siku tatu. Mvua hizo kubwa zilizoiathiri Morocco zimesababisha madhara na uharibifu katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na mji wa Tetouan wa kaskazini mwa nchi hiyo na mji wa milimani wa Tinghir.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, Safi ni mji Safi, unaopatikana kwenye ufuo wa Atlantiki ya Morocco zaidi ya kilomita 320 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Rabat. Mji wa Safi pia ni kitovu kikuu cha sekta muhimu ya uvuvi na madini nchini Morocco.
Mji huo wenye wakazi zaidi ya 300,000 ni makazi ya kiwanda kikubwa cha usindikaji wa fosfati.
Video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zmeonyesha magari yakiwa yamekwama katika madimbwai ya maji huku mitaa ya mji wa Safi ikiwa imefurika kwa maji.
Mabadiliko ya tabianchi yamepelekea mifumo ya hali ya hewa nchini Morocco kuwa vigumu kutabirika. Mafuriko yameripotiwa kuiathiri Morocco wiki hii baada ya watu 22 kupoteza maisha baada ya majengo mawili kuporomoka katika mji wa Fez nchini humo.