Naibu Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Salome Makamba, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuwapa ajira wazawa katika utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi, hususan katika kipindi hiki cha mwisho cha ujenzi.
Makamba ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya pamoja na Naibu Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Ruth Nankabirwa, waliotembelea eneo la Chongoleani mkoani Tanga kujionea maendeleo ya mradi huo.
Kwa mujibu wa taarifa za mradi, ujenzi umefikia asilimia 86 na unatarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka huu, huku ukiwa tayari umetoa ajira kwa zaidi ya wananchi 9,000 kutoka mkoani Tanga na maeneo mengine.
✍ Mariam Shedafa
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates