Serikali imesema uwekezaji wa zaidi ya Shilingi Bilioni 280 katika miradi mbalimbali ya umeme jijini Dar es Salaam unalenga kumaliza hali ya kukatika kwa umeme hata panapotokea hitilafu kwenye moja ya vyanzo vya umeme vilivyopo ndani ya mkoa huo.

Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya kupoza na kuzalisha umeme vilivyopo Dar e Salaam, Waziri wa Nishati Deogratius Ndejembi amesema mkoa huo unatumia karibu megawati 750 huku Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange akisema uwekezaji huo ni sehemu ya zaidi ya Shilingi Trilioni 15 zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme nchini.

Mhariri @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *