Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) inaendelea kuliheshimisha Taifa kwa kunyakua Tuzo ya Afrika ya Mifumo ya Kijiditali, baada ya kuonyesha ubunifu na ubora wa hali ya juu katika mashindano yaliyoshirikisha taasisi mbalimbali kutoka barani Afrika.

Mashindano hayo yalifanyika mapema mwezi Desemba 2025 katika mji wa Manzini, mji mkuu wa Eswatini, sambamba na Mkutano wa 44 wa Wataalamu wa Usimamizi wa Utawala katika Utumishi wa Umma barani Afrika, unaoandaliwa na Jumuiya ya African Association of Public Administration and Management (AAPAM).

Katika ushindani huo mkali wa mapendekezo 49 kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Tanzania kupitia TFRA iliibuka nafasi ya tatu kwa pamoja na Afrika Kusini, huku Zambia ikichukua nafasi ya kwanza katika kipengele cha Ubunifu Bora wa Mwaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *