Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amewaagiza wenyeviti wa vitongoji na mitaa mkoani humo kuimarisha juhudi za uhamasishaji, usimamizi na ufuatiliaji kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye umri wa kwenda shule, ili kuhakikisha watoto wote wanaandikishwa na kuanza masomo kwa wakati na kuongeza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuhakikisha haki ya mtoto ya kupata elimu inazingatiwa kikamilifu.

Ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na wananchi katika moja ya ziara zake za kikazi, iliyofanyika katika Kijiji cha Kitelewasi, Kata ya Irole, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, ambapo amewataka wazazi na walezi kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wao na kushirikiana na viongozi wa ngazi za chini katika kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanapata fursa hiyo bila kikwazo chochote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *