Dar es Salaam. Waimbaji  maarufu wa muziki wa Injili nchini, Rose Mhando na Upendo Nkone, ni kati ya wasanii watakalipamba tamasha ya Power Day Experience (PDX) linalotarajiwa kufanyika Januari 16,2026 Wilaya ya Kigamboni.

Hayo yamesemwa na muandaaji kiongozi wa tamasha hilo,Harun  Laston ’Zoravo’ alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo ambalo itakuwa mara yake ya kwanza kufanyika wilayani humo na litafanyika viwanja vya Mjimwema.

Ukiacha Mhando na Nkone, wengine watakao kuwepo ni Obby Alpha, John Kavishe, Henrick Mruma na Eliah Mtishibi.

Zoravo amesema lengo la kufanya tamasha hilo ambalo ni mwaka wake wa tatu tangu lililipoanza, imetokana na mara nyingi watu wa Kigamboni kuvuka maji na kuihudhuria upande wa pili, hivyo sasa hivi wameona wawafuate walipo.

Mratibu wa Tamasha la PDX, Harun Laston,akiwa anazungumza katika mkutano na waandishi wa habari

“Kwa kulitambua hilo ndio maana tukaja na kaulimbiu ya “Na tuvuke mpaka Ng’ambo’ ambapo siku hiyo  pamoja na mambo mengine,  watu wataruka, wataimba pamoja na kuomba.

“Kwani kuna watu wengine wanajua kuimba ni kuburidika tu, lakini uimbaji pia ni uponyaji na siku hiyo watakaohudhuria watashuhudia hilo kwa kuwa utakuwa usiku wa kihistoria,”amesema mratibu huyo.

Naye mwimbaji John Kavishe, amesema katika kizazi cha sasa ambacho kina mmomonyoko mkubwa wa maadili, kuna haja ya kuwaweka vijana karibu na Mungu.

Kutokana na hilo, Kavishe amesema hategemei wazazi  au walezi kuwakataza watoto wao kwenda kushiriki katika tamasha hilo la kusifu na kuabudu.

Julieth Madale mmoja wanakamati, amesema ili kuwarahisishia watu kufika katika tamasha hilo, kutakuwepo na usafiri ikiwemo katika vyuo vikuu vilivyopo jijini Dar es Salaam na hakutakuwepo na kiingilio zaidi ya miguu ya mtu na muda wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *