#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji linapenda kutoa taarifa ya kukamatwa kwa watuhumiwa 8 ambao ni bodaboda huko katika Kijiji cha Kiwambo Kata ya Kitomondo Tarafa ya Kisiju wilayani Mkuranga kwa tuhuma za kuharibu mali, ambapo waliharibu kwa kuvunja vioo vya mbele vya malori 16 na mabasi ya kubeba abiria 2.
Tukio hjlo limetokea Januari 16, 2026 wakati madereva bodaboda hao wakielekea kumpumzisha bodaboda mwenzao huko Kijiji cha Kiwambo wilayani Mkuranga ambaye inasadikika alifariki dunia baada ya kupata ajali ya kugongwa na gari huko Keko jijini Dar es Salaam.
Watu hao walifanya matukio hayo kwenye magari waliyokuwa wanakutana nayo njiani kwa kuvunja vioo vya mbele kwa kurusha mawe na vipande vya tofali huku wakiwa wanakimbia kwa kutumia pikipiki.
Pikipiki tatu walizokuwa wanatumia kama usafiri wao kutekeleza uhalifu huo zimekamatwa ambazo ni: MC 574 EQP, MC 496 FJG na nyingine yenye chassis No. BX2SWG66853G7 zote aina ya boxer.
Watuhumiwa hao wanashikiliwa katika kituo cha Polisi Mkuranga kwa mahojiano zaidi na watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.