
Jeshi la Mali (FAMa) limeeleza kuwa liimefanya mashambulizi ya anga dhidi ya makundi ya kigaidi kusini-magharibi mwa nchi hiyo, na kulenga “harakati kubwa” ya wanamgambo karibu na eneo la Mourdiah.
Taarifa ya Jeshi la Mali imesema kuwa mashambulizi hayo yalifanywa kama sehemu ya operesheni ya upelelezi yakilenga makundi ya waasi kusini mashariki mwa kambi ya Mourdiah. Hata hivyo jeshi la Mali halikufafanua ni makundi gani ya kigaidi yalilengwa.
Mali imekuwa na tatizo la usalama tangu mwaka 2012, lililochochewa na vuguvugu la watu wanaotaka kujitenga na mashambulizi ya kigaidi, hasa katika mikoa ya kaskazini na kati mwa nchi hiyo.
Mwezi Desemba mwaka 2024, makundi yanayobeba silaha yaliyojitenga yalitangaza kuundwa harakati ya la Azawad Liberation Front (FLA) inayotaka kuwa huru baadhi ya mikoa ya kaskazini mwa Mali.
Muungano huo una Baraza Kuu la Umoja wa Azawad (HCUA), Vuguvugu la Kitaifa la Ukombozi wa Azawad (MNLA), na vikundi vya waasi vya Azawad Arab Movement (MAA) na kundi la Kujilinda la Imghad Tuareg na waitifaki wao, (GATIA).
Serikali ya Mali inayatambua makundi hayo pamoja na mtandao wa kigaidi wa al Qaida na harakati ya FLM kuwa makundi ya kigaidi.