Dar es Salaam. Mamia ya mashabiki wa Espérance Sportive de Tunis wameuteka Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa shangwe na vaibu lao wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba SC.
Tangu dakika za awali za mchezo huo, mashabiki wa Espérance walionekana kutawala kwa kelele, nyimbo na shangwe kila wakati, wakitoa presha kwa wapinzani wao Simba ambao mashabiki wao walionekana kusikilizia zaidi matukio ya mchezo kabla ya kushangilia.
Kutokana na joto la jijini Dar es Salaam, baadhi ya mashabiki wa Espérance walionekana kuvua mashati lakini hilo halikuwazuia kuendelea kuisapoti timu yao, wakipeperusha bendera na kuimba.
Ushabiki huo ulionekana kuchochewa na historia kubwa ya mafanikio ya Espérance katika soka la Afrika, ambapo klabu hiyo ni miongoni mwa timu zilizofanikiwa zaidi, ikiwa imetwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mara nne katika miaka ya 1994, 2011, 2018 na 2019.
Baadhi ya wachezaji wa Esperance de Tunis, wakipasha misuli kabla ya mchezo kuanza. Picha na Esperance
Mbali na mataji ya Afrika, Espérance pia ni klabu iliyotawala soka la Tunisia kwa miaka mingi, ikijizolea ubingwa wa ligi mara 34.
Simba SC: Kassali; Kante, Kapombe (C), Oura, Kagoma; De Reuck, Chama, Gueye; Nangu, Kibabage, Kibu.
(Akiba: Abel, Duchu, Sowah, Toure, Naby, Morice, Mwalimu, Loemba, Mpanzu.)
Esperance Sportive de Tunis: Ben Said; Keita, Laifi, Jelassi, B. Hmida (C), Konaté, Onuche, Tka; Yan Sasse, Diakité, Diarra.
(Akiba: Mechiche, Guemichi, Florent, Msakni, Rafa, Kouceila, Jebali, Jabri.)