Meneja wa Mradi wa Railway Children Afrika, Kidaha Mohamed, amesema watoto wa mitaani hujikuta katika mazingira hayo kutokana na changamoto za kifamilia na kijamii, si kwa hiari yao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, amesema hali hiyo inapaswa kuifanya jamii kuchukua jukumu la kuwalinda na kuwajali watoto hao ili kuepuka hatari zinazoweza kuathiri maisha yao.

Ameongeza kuwa watoto wa mitaani wanahitaji ulinzi, malezi na fursa sawa kama watoto wengine ili kuwawezesha kurejea katika maisha ya kawaida.

✍Ibrahimu Kilumbo
@elesia_haule

Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *