Baada ya Jenerali Fannie Masemola kuripoti mahakamani kwa muda mfupi mjini Pretoria mapema wiki hii, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza kumsimamisha kazi “kama hatua ya tahadhari, hadi kesi itakapofungwa,” Alhamisi, Aprili 23.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Johannesburg, Valentin Hugues

Tangazo hilo lilitarajiwa nchini Afrika Kusini: siku ya Alhamisi, Aprili 23, Rais Cyril Ramaphosa alitangaza kusimamishwa kazi kwa mkuu wa polisi, Fannie Masemola, ambaye ameshtakiwa katika kesi ya ufisadi inayohusishwa na zabuni tata yenye katika sekta ya afya.

“Kwa kuzingatia uzito wa mashtaka haya na jukumu muhimu ambalo Kamishna wa Polisi wa anapaswa kuchukuwa katika mapambano dhidi ya uhalifu, nimekubaliana na Jenerali Masemola kwamba atasimamishwa kazi kama hatua ya tahadhari hadi jambo hilo litakapotatuliwa,” rais alisema.

Tangazo hilo lilikuja baada ya Jenerali Masemola kufika  kwa muda mfupi mbele ya mahakama ya Pretoria mapema wiki hii. Ingawa mahakama imeamua kuahirisha kesi hiyo, jina la Fannie Masemola limekuwa likigonga vichwa vya habari katika magazeti ya Afrika Kusini tangu kushtakiwa kwake mwezi uliopita na hivyo kuzua mjadala kuhusu mustakabali wake kama mkuu wa polisi wa Afrika Kusini.

Mfano mwingine wa ufisadi ndani ya jeshi la polisi la Afrika Kusini Jenerali Masemola, ambaye anasema hata hatia na hapo awali alikataa kujiuzulu, anakabiliwa na mashtaka manne, yote yanayohusiana na usimamizi wa fedha za umma. Anashutumiwa hasa kwa kuhusika katika utoaji wa mkataba mnono—unaoshukiwa kuwa wa ulaghai—kwa “Cat” Matlala, mhalifu anayejulikana sana na polisi na ambaye kwa sasa yuko gerezani.

Kusimamishwa kwake kazi pia kunaonyesha, kwa mara nyingine tena, kiwango cha ufisadi kinachowakumba polisi wa Afrika Kusini. Tangu Waziri wa Polisi apewe likizo mwezi Julai mwaka uliyopita, tume ya uchunguzi imepewa jukumu la kufichua uingiaji wa mitandao ya uhalifu ndani ya taasisi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *