
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kwamba mauaji ya kutisha yaliyofanywa na jeshi utawala vamizi la Israel huko kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, ambayo yamewalenga moja kwa moja watoto, ni kielelezo kipya cha kuendelea vita vya mauaji ya kimbari na maangamizi ya kizazi katika maeneo mbalimbali ya Ukanda huo.
Hazem Qassem, msemaji wa harakati ya Hamas amesema kwamba shambulio la ndege isiyo na rubani dhidi ya kundi la raia katika uwanja wa umma katika Mradi wa Beit Lahia kaskazini mwa Gaza, ambalo limeua raia watano, wakiwemo watoto watatu, ni uhalifu mpya katika mwendelezo wa mauaji ya kimbari na ukiukwaji unaoendelea na sheria za kimataifa.
Msemaji wa Hamas pia amesema kwamba uhalifu huu ni ishara ya kushindwa kile kinachoitwa Bodi ya Amani kuwalazimisha wavamizi kuacha ukiukaji huo wa sheria au kutekeleza majukumu yao ndani ya mfumo wa makubaliano yaliyopo.
Ameongeza kuwa uhalifu huu unaonyesha wazi kwamba jeshi la utawala wavamizi linahusika moja kwa moja katika mauaji ya kimbari na ukiukaji wa sheria za kimataifa na za kibinadamu.