Rais wa Lebanon ameeleza kusikitishwa kwake na mauaji ya mwandishi wa habari wa nchi hiyo na kujeruhiwa mwandishi mwingine wa habari katika shambulio la utawala wa Kizayuni wa Israel kusini mwa Lebanon, akitangaza kwamba lengo la uhalifu huu ni jitihada za utawala wa Israeli za kutaka kuficha uhalifu wake.

Rais wa Lebanon, Joseph Aoun, amesema kwamba kushambuliwa kwa makusudi na moja kwa moja wafanyakazi wa vyombo vya habari ni jaribio la utawala wa Israel la kuficha uhalifu na jinai zake dhidi ya Lebanon.

Amesisitiza kwamba vitendo hivi vinatambuliwa kuwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu uliopigwa marufuku na sheria na kimataifa. Vilevile amesisitiza kuwa sheria za kimataifa zinaiwajibisha jamii ya kimataifa kuingiia kati kwa shabaha ya kuzuia uhalifu huo.

Aoun atuma salamu zake za rambirambi kwa familia na wafanyakazi wa gazeti la Al-Akhbar kutokana na kuuawa shahidi mwandishi wa habari wa Amal Khalil katika mji wa Al-Tayri, na kumuombea ahueni mwandishi mwingine aliyeandamana naye, Zeinab Faraj, ambaye amejeruhiwa katika shambulizi ya Israel.

Wakati huo huo, Peyman Jabelli, mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), ametuma ujumbe katika ujumbe kwa mnasaba wa kuuawa shahidi mwandishi wa habari wa Lebanon, Amal Khalil akiswema: Hofu kubwa inayousumbua utawala wa Kizayuni ni kufichuliwa ukweli. Ndiyo maana unawashambulia waandishi wa habari mara kwa mara.

Mkuu wa IRIB ameongeza: Mara hii, damu ya mwandishi wa habari wa Lebanon aliyeuawa shahidi, Amal Khalil inaangazia hakika na ukweli. Ukweli unaoitwa kubakia hai Muqawama na kifo cha taratibu cha utawala wa kihalifu wa Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *