Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo imempa tuzo malum Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo kwa kutambua mchango wake wa kiuongozi katika kuendeleza sekta ya biashara.
Mpogolo amekabidhiwa tuzo hiyo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2026 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), uliofanyika katika Soko Kuu la Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, tarehe 25 Aprili 2026.
Akishukuru baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema “Kwa niaba ya wenzangu wote naipokea kwa unyenyekevu mkubwa kama ishara ya imani na ushirikiano wenu na napenda kumshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kujenga na kuimarisha mazingira rafiki ya biashara nchini.”
Mbali ya shukrani hiyo, Mpogolo ameahidi kuendeleza ushirikiano kwa karibu zna wafanyabiashara hao ili kukuza sekta ya biashara na maendeleo ya Kariakoo na Taifa .
Mhariri @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)