Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, imebaini kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo sasa inashika nafasi ya tano duniani kwa idadi ya wakimbizi, huku hali ya kibinadamu ikiendelea kuzorota.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa UNHCR, DRC ina zaidi ya wakimbizi wa ndani milioni 6.4, wengi wao wakiwa katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo ambako mizozo ya kivita imeendelea kwa muda mrefu.

Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka hadi kufikia milioni 9 ifikapo mwisho wa mwaka huu iwapo hali ya usalama haitaimarika, hii inaifanya DRC kuwa miongoni mwa nchi zilizoathirika zaidi baada ya Sudan, Syria, Afghanistan na Ukraine.

Ripoti hiyo pia inaonyesha ongezeko kubwa wa njaa, ambapo raia mmoja kati ya wanne anakabiliwa na uhaba wa chakula, huku zaidi ya watu milioni 6 wakikumbwa na utapiamlo, hali ambayo haijapungua kwa zaidi ya miaka 20.

UNHCR inaonya kuwa mahitaji ya misaada ya kibinadamu yamefikia takriban dola bilioni 1.4 ili kuwasaidia zaidi ya watu milioni 7 walio katika hatari kubwa zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *