Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, ameteuliwa na chama chake cha CNDD-FDD kuwa mgombe wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ndayishimiye mwenye umri wa miaka 57 hivi sasa, ameongoza taifa hilo tangu mwaka 2020, kufuatia kifo cha mtangulizi wake Pierre Nkurunziza.

Kupitia ukurasa wake wa X, chama hicho kimesema Ndayishimiye ndie chaguo lao kuwania kuteuliwa kuongoza kwa muhula wa miaka 7.

Tangazo hilo linatolewa wakati huu mpaka sasa tume ya uchaguzi nchini humo ikiwa haijatangaza terehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo.

Tangu achukue madaraka, Ndayishimiye amekuwa akisitasita kati ya kufungua serikali ili kupunguza ushawishi wa majenerali wenye nguvu au kuongeza  udhibiti wa chama hicho madarakani.

Licha ya Ahadi ya kuifungua nchi hiyo na kuruhusu uhuru wa maoni na Habari, mashirika ya kutetea haki za binadamu ikiwmo umoja wa Mataifa, wamemnyooshea kidole Ndayishimiye kwa kuendelea vitendo vya ukandamizaji dhidi ya wakosoaji wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *