Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ya kutaka kuunganishwa katika kesi ya mgawanyo wa mali iliyofunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohamed, pamoja na wenzake wawili.
Wengine katika kesi hiyo ni Ahmed Rashid Khamis na Maulidah Anna Komu (marehemu).
Uamuzi huo wa awali umesomwa na Msajili, ambapo mahakama imekataa kumuunganisha Lissu, ikieleza kuwa ingawa yeye ni Mwenyekiti wa Chadema, aliwasilisha maombi hayo kwa nafasi yake binafsi na si kwa niaba ya uenyekiti wa chama, hivyo hana maslahi ya moja kwa moja katika kesi hiyo.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)