#HABARI: Mtendaji wa Kijiji cha Idiwili Halmashauri ya Mbozi Mkoani Songwe amejikuta katika wakati mgumu baada ya wananchi wa Kijiji hicho kutoa malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe ndugu Jabiri Makame wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Tuhuma zilizotolewa na wananchi zinahusisha kupokea fedha shilingi laki 510,000 kupitia simu yake zinazodaiwa kuwa ni mchango wa mwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya kijiji, kukusanya michango ya wananchi shilingi mil 4,500,000 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Ilomba, pamoja na tuhuma za kununua na kulima mashamba yaliyokuwa yakimilikiwa na mtuhumiwa wa mauaji hali ya kuwa mtuhumiwa huyo ametoroka hivyo kujenga mashaka kwa wananchi kwamba huenda anajua aliko mtuhumiwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe aliagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza tuhuma hizo za rushwa huku Jeshi la Polisi wakitakiwa kuendelea na uchunguzi wa tuhuma zilitolewa za kulima kwenye shamba mtuhumiwa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *