Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema mkanda mzima wa tukio la mauaji ya kijana James mwanafunzi wa chuo aliyeuawa kisha kichwa chake kutoweka itawekwa hadharani hivi karibuni mahakamani
Kwa mujibu wa RC Chalamila, tayari Jeshi la Polisi imechunguza na kubaini sababu ya kifo hicho.
Chalamila amesema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Jumanne Murilo katika taarifa yake imeonyesha kijana huyo ameuawa kutokana na imani za kishirikina ambako mganga wa kienyeji anadaiwa kuchukua maini, figo na sehemu ya kichwa na kwenda kuzika pembeni mwa nyumba yake.
“Mkanda mzima tutausikia mahakamani, siyo lazima tuseme kila kitu katika uchunguzi,'” amesisitiza RC Chalamila wakati wa ziara yake Jijini Dar es Salaam.
(Feed generated with FetchRSS)