Zaidi ya migogoro elfu mbili na miatatu sabini na kati yake migogoro 331 imetatuliwa katika siku 10 za kampeni ya msaada wa kisheria awamu ya pili mkoani Shinyanga ambapo migogoro mingi ni migogoro inayohusiana na masuala ya ardhi,madai kati ya mtu binafisi na taasisi na matunzo kwa upande wa watoto.
Mratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria mkoa wa Shinyanga Raurent Burilo amebainisha hayo wakati akizungumza na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julious Mtatiro baada ya kutembelea mabanda yanayotoa huduma za msaada wa kisheria katika manispaa ya Shinyanga ili kujionea mwenendo wa huma hiyo.
Amesema kuwa zaidi ya watu lakitatu nanusu mkoani humo wamefikiwa na bado kampeni hiyo inaendelea katika halimashari zote za mkoa wa Shinyanga hadi may 20 mwaka huu.
Akizungumza katika eneo hilo mkuu wa wilaya ya Shinyanga amesema uhitaji wa elimu ya masuala mbalimbali hususani ya kisheria na migogoro ya ardhi kwa wananchi ni mkubwa ndio maana serkali imeendelea kutengeneza namna mbadala ya kuwafikia wananchi katika maeneo yao kama ilivyo katika kampeni ya msaada wa kisheria ili kuendelea kuwapatia elimu na kutatua migogoro.
Rai zaidi inatolewa wa wakazi wa Shinyanga kuendelea kujitokeza katika kampeni ya msaada wa kisheria ili wapate huduma ikiwemo elimu ya masuala ya kisheria na utatuzi wa migogoro.

(Feed generated with FetchRSS)
