#HABARI: Taharuki imeibuka katika Mtaa wa Mazimbu Darajani, Kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro baada ya kijana mmoja Sadiki Mr…#HABARI: Taharuki imeibuka katika Mtaa wa Mazimbu Darajani, Kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro baada ya kijana mmoja Sadiki Mr…

#HABARI: Taharuki imeibuka katika Mtaa wa Mazimbu Darajani, Kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro baada ya kijana mmoja Sadiki Mrisho maarufu kama Kipanya, kudaiwa kufariki dunia kwa kuchomwa moto, nduguze kuandaa msiba nyumbani kwake na baadaye kugundulika marehemu hakuwa yeye, badala yake Sadiki aliyetajwa alikuwa akishikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi Morogoro akituhumiwa kuendesha bajaji ilitotumika kufanya jinai.

ITV imefika nyumbani kwa Sadiki Mrisho na kuzungumza na kaka yake Abdurazak Mrisho, aliyeeleza kwa kina tangu taarifa za msiba na ufuatiliaji wa mwili hadi kugundua hakuwa amefariki bali alikuwa akishikiliwa kituo kikuu cha polisi.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mazimbu Darajani, Bw. Evod John, ameeleza hatua alizochukua baada ya kupokea taarifa za msiba huku Abdulrazak akimuondoa mdogo wake kwenye tuhuma za wizi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Andrew Kantimbo akizungumza na ITV kwa njia ya simu, amekiri kushikiliwa kwa kijana Sadick Mrisho kwa tuhuma za wizi wa bajaji tangu Mei 13, mwaka huu, na wakati mahojiano yakiendelea, ndugu walipata taarifa za kijana mwingine kuwa yupo chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na walikwenda kuchukua mwili waliodhani ni wa ndugu yao kwa maziko.

Hata hivyo, Mei 16 walipata taarifa zaidi kuwa ndugu yao yuko hai na anahojiwa polisi na kweli walimkuta na kumtambua, na mwili kurudishwa hospitali.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *