Jiongeze: Mfume dume kama tatuu umejikita akiliniJiongeze: Mfume dume kama tatuu umejikita akilini

Dar es Salaam. Wanawake wanaojiuza hupewa majina mabaya. Kama malaya, changudoa, vicheche, milupo na mengineyo. Wanaume ambao ndo wanunuzi wakuu, huonekana ni wajanja wa ‘tauni’ wanaojua chimbo za wajasiriamili hao wa kike. Kifupi ni sifa njema kwao.

Thamani ya bikira ni kwa mtoto wa kike tu, wa kiume akitoka na ‘demu’ umri wa shangazi yake hugeuka kashujaa flan hivi katika jamii. Pindi binti akipata ujauzito wazazi hukasirika sana, wazazi wa kijana aliyempa huo ujauzito hufurahia na kuona kidume.

Wazazi hawapendi mtoto wa kike awe na “boifrendi’, ila wa kiume akiwa na ‘gerofrendi’ huchekelea. Ndoa ikivunjika lawama zote kwa mwanamke, mara kaachika, ndoa imemshinda ama hakufundwa. Hata kama huyo mwanamke ndiye aliyemuacha mwanaume.

Dada akiona dogo lake la kiume lina ‘gerofrendi’ hakasiriki. Lakini dogo la kiume likiona dada yake ana ‘boifrendi’ hukasirika sana. Kaka anaweza kumtuma dada akamuunganishe na rafiki yake. Lakini ni vita kubwa kwa kaka mtu kutoa pasi kwa dada apate masela.

Mwanaume akiwa na wapenzi wengi ni rijali, mwanamke akiwa na wapenzi wawili tu ni malaya. Huko uswahilini kwetu hata dada ambaye tayari kazalishwa, bado ndugu wa kiume huumia wakiona yupo na kidume. Na ‘samtaimu” ngumi zinatembea.

Hii ni athari ya mfumo dume. Ni wazi Kiafrika, suala hili ni kama mtu aliyejichora tatuu, haifutiki. Achana na ‘jenda balansi’ katika ajira na ushirikishwaji kwenye maamuzi mengi. Pia vitabia hivi vidogo vidogo vinautukuza sana mfumo dume.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *