Mbunge wa Jimbo la Hai, Saashisha Mafuwe, amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanya mabadiliko makubwa tangu ilipo anzishwa miaka 30 iliyopita.
Kwa mujibu wabunge huyo, mabadiliko hayo yamechangia kuleta utulivu na kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara nchini.
Akizungunza Jijini Dodoma mbunge huyo amesema maboresho yanayofanywa na taasisi hiyo yameongeza uelewano na wafanyabiashara jambo linalowapa fursa ya kutekeleza shughuli zao katika mazingira yenye utulivu na kujiamini.
Mafuwe amesema TRA imeendelea kuonesha dhamira ya kujenga ushirikiano na walipakodi kwa kusikiliza maoni yao, kuboresha utoaji wa huduma na kuweka mifumo inayorahisisha utekelezaji wa majukumu ya kodi kwa kuongeza imani ya wafanyabiashara kwa taasisi hiyo na kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi.
Aidha, amewataka wafanyabiashara kuendelea kushirikiana na TRA kwa kutekeleza wajibu wao wa kulipa kodi kwa hiari na kwah wakati, akisisitiza kuwa mapato ya kodi ndiyo msingi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi.
(Feed generated with FetchRSS)