Wanafunzi wa kidato cha pili na kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kibamba wamejengewa uelewa kuhusu ugonjwa wa Siko Seli (Selikundu).

Katika tukio hilo vipimo 150 vya uchunguzi wa awali viliandaliwa na Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Siko Seli kwa ajili ya wanaohitaji kupima kwa hiyari ambako wanafunzi 36 wa wamefanyiwa uchunguzi na sita kati yao wamebainika kuwa wabebaji wa kinasaba [AS] 30 wakikutwa na vinasaba vya kawaida [AA].

Jumuiya ya Watu Wanaoishi na ugonjwa wa Siko Seli Tanzania (SCDPCT) imeadhimisha siku hiyo kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, Asnath Mohamed amewashukuru madaktari pamoja na mashujaa wa Siko Seli kwa kufika shuleni hapo na kuwapatia elimu pamoja na huduma ya uchunguzi wa kinasaba.

Akitoa ushuhuda wake, shujaa wa Siko Seli kutoka SCDPCT, Julius Joseph amesema bado jamii inaamini watu wenye Siko Seli hawezi kuishi zaidi ya miaka 18 lakini yeye amesoma na sasa ni afisa utabibu

Naye Mtaalamu wa Sayansi za Maabara wa MNH Wilson Hape, amesema ni muhimu wananchi kupima mapema kabla ya kuamua kuanzisha familia

Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu isemayo, “Tuchukue Hatua kwa Usawa: Kuongeza Nafasi ya Kuishi kwa Wagonjwa wa Siko Seli.”

#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *