Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw.Mohamed Salum, amesema kuwa usafiri wa meli ya MV Liemba una umuhimu mkubwa kwa wananchi wanaotegemea huduma za usafiri wa majini katika ukanda wa Ziwa Tanganyika, huku akieleza kuwa meli hiyo itakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Wananchi.
Salum ametoa kauli wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa meli ya MV Liemba mjini Kigoma katika maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani yanayoendelea mkoani humo.
Vilevile amesema kuwa wananchi wengi wa maeneo yanayozunguka Ziwa Tanganyika wanategemea sana usafiri wa majini kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi, hivyo kukamilika kwa ujenzi wa meli hiyo kutasaidia kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali.
Amesema kuwa katika mkoa wa Kigoma, MV Liemba itaendelea kuwa nyenzo muhimu ya kuchochea shughuli zayou biashara, kuunganisha jamii na kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi wa ukanda huo.
Sambamba na hayo Salum amesema uwekezaji unaofanyika katika kuboresha meli hiyo unaonesha dhamira ya Serikali ya kuimarisha sekta ya usafiri wa majini na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zinazochangia ukuaji wa uchumi wa bluu nchini.
Ziara hiyo iliyofanywa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania TASAC,ni sehemu ya shughuli za Maadhimisho ya Siku ya Mabaharia ambayo yanalenga kutambua mchango wa mabaharia na wadau wa sekta ya usafiri wa majini katika maendeleo ya Taifa.
Mkurugenzi huyo wa TASAC Mohamed Salum ameyasema hayo Katika ziwa Tanganyika Jijini Kigoma,wakati akikagua Meli hiyo ya MV Liemba.
#StarTvUpdate
(Feed generated with FetchRSS)