Chama cha ACT Wazalendo kimeendelea kuwatoa hofu wananchi kuhusu ushiriki wake katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, kikieleza kuwa bado kinaendelea na mchakato wa mazungumzo kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho unaozingatia maslahi ya Zanzibar na wananchi wake.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara, Isihaka Mchinjita, wakati akizungumza na waandishi wa habari, siku chache baada ya chama hicho na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kusaini tamko la pamoja la maridhiano ya kisiasa Zanzibar.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *