Vyama 14 vya kisiasa ambavyo vimikutana mwishoni mwa wiki hii huko Ibadan, kusini magharibi mwa Nigeria, vilikubaliana kusimamisha wagombea kutoka vyama hivyo katika ngazi zote za uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Januari mwakani, ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa urais ambapo watatangaza jina la mgomea mmoja. Lengo: kupinga Bunge kutawaliwa na wabunge kutoka chama cha APC cha rais Bola Ahmed Tinubu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Abuja, Moïse Gomis

vyama hivi 14 ambavyo vilikutana huko Ibadan, kusini magharibi mwa Nigeria, viliahidi kuunganisha nguvu pamoja kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 ili kupinga Bunge kutawaliwa na chama cha APC.

Mpango huu unakuja huku magavana kadhaa, wabunge, na madiwani walijiunga na kambi ya wengi ya rais  katika miezi ya hivi karibuni, wakiamini wazo kwamba Rais Bola Ahmed Tinubu anaweza kuibuka kama mgombea wa makubaliano katika uchaguzi wa urais wa 2027 na kushinda bila kupingwa—mtazamo ambao vyama 14 vinavyohusika vinafutilia mbali.

Katika kile wanachokiita “Azimio la Ibadan,” vyama hivi vinaishutumu APC kwa kudhoofisha demokrasia ya vyama vingi na vinakusudia kupinga matarajio yake ya madaraka kamili kwa kusimamisha wagombea katika ngazi zote za uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwaka ujao. Majadiliano yanaendelea hata kuwasilisha mgombea mmoja katika uchaguzi wa urais, ambaye ataungwa mkono na muungano mzima.

Ajenda ya pointi tisa

Vigogo kadhaa wa siasa za Nigeria walionekana katika mkutano huu siku ya Jumamosi na Jumapili. Miongoni mwao ni Makamu wa Rais wa zamani Atiku Abubakar, Gavana wa zamani wa Kano Rabiu Kankwoso, Waziri wa zamani wa Uchukuzi Rotimi Amaechi, na kiongozi wa chama cha PDP, Kabiru Turaki.

Peter Obi, ambaye alishika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2023, ni mmoja wa wachangiaji wakuu wa maazimio yaliyojumuishwa katika ajenda ya pointi tisa. Madai mawili makuu ni: kwanza, mapitio ya Bunge ya vifungu vya sheria ya uchaguzi ya mwaka 2026, ambayo vyama hivi 14 vinaamini vinaweza kudhoofisha uaminifu wa uchaguzi; na pili, kuahirishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi hadi mwisho wa mwezi Julai kwa tarehe ya mwisho ya kuandaa kura za mchujo za vyama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *