Jamii imetakiwa kuendelea kushirikiana katika makuzi na malezi ya watoto na vijana ili kujenga jamii bora yenye maadili, amani na maendeleo endelevu.

‎Wito huo umetolewa na Katibu wa Taasisi ya MIFTAH SALAAM, Idrisa Modo, wakati wa kongamano la amani lililoandaliwa kwa lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo, hususan vijana, kwa ajili ya kujadili masuala yanayohusu amani, mshikamano na maendeleo ya jamii.

‎Amesema ushirikiano wa wazazi, viongozi wa dini, serikali na wadau wengine wa maendeleo ni muhimu katika kuhakikisha vijana wanapata malezi bora yatakayowajengea uwezo wa kuwa raia wema na wenye mchango chanya kwa taifa.

‎Aidha, Modo amesema taasisi hiyo ina mpango wa kuufikia mkoa mzima wa Tanga kupitia shughuli mbalimbali za elimu na uhamasishaji zinazolenga kuimarisha amani, maadili mema na maendeleo ya vijana.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *