Utamaduni unaendelea kuvuka mipaka ya mikoa nchini, ukichochewa na kuenea kwa lugha ya Kiswahili, maboresho ya miundombinu na shughuli za kiuchumi. Mfano wa hali hiyo ni ngoma ya asili ya Dogoli kutoka Mkoa wa Ruvuma ambayo sasa imepata umaarufu mkubwa Mkoa wa Rukwa.
Kikundi cha Coins kimekuwa kivutio kikubwa kutokana na umahiri wake katika kucheza ngoma hiyo, hali iliyomvutia Sammy Kisika kukitembelea kikundi hicho kilichoundwa mwaka mmoja uliopita. Ziara hiyo imelenga kufahamu siri ya ngoma hiyo kutoka Ruvuma kupata mapokezi makubwa na kupendwa Rukwa.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)