Kujifunza lugha za mataifa mbalimbali ni fursa inayoweza kufungua milango ya ajira, biashara na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.
Hilo limethibitishwa na Mtanzania Elias Masanja, ambaye baada ya kujifunza lugha ya Kirusi sasa anafanya kazi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi kama Afisa wa Utalii, Uwekezaji na Biashara.
Akiwa nchini Urusi, mwandishi wetu Upendo Michael alikutana na Elias Masanja, ambaye pamoja na majukumu yake ya kidiplomasia pia hushiriki katika ukalimani kwenye mikutano mbalimbali inayowakutanisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Urusi.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)