Hatimaye waandishi wa habari wakongwe nchini waliokidhi vigezo wataanza kupatiwa Ithibati ya Maisha kama njia ya kutambua na kuthamini mchango wao katika kuendeleza sekta ya habari.

Hatua hiyo imekuja baada ya Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) kuzindua rasmi mwongozo wa utambuzi wa kundi hilo, unaolenga kuweka utaratibu wa kuwapatia ithibati waandishi waliotumikia taaluma hiyo kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Upendo Michael, uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB).

#AzaTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *