Takribani watu 930 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Hiyo ni kwa mujibu wa Wizara ya Afya nchini humo.

Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema katika taarifa yake kwamba, vifo hivyo vimerekodiwa miongoni mwa visa 2,344 vya maambukizi vilivyothibitishwa hadi siku ya Jumamosi. Vifo vipya vilirekodiwa katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, idadi ya juu kabisa kuwahi kurekodiwa kwa siku moja.

Ongezeko la vifo linaripotiwa huku hofu za usalama zikizuia utoaji wa huduma katika jimbo la Ituri lililoathiriwa zaidi.

Mamlaka zilisema Jumamosi kwamba karibu vituo 12 pamoja na watumishi wa afya wameshambuliwa tangu mlipuko huo ulipotangazwa katikati ya Mei.

Mkurugenzi wa Operesheni wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, ICRC, Bruno Michon, anasema mlipuko huo unaenda kasi kuliko uwezo wa kuudhibiti. “Sasa ni miezi miwili tangu mlipuko huu uanze. Tangu tarehe 15 Mei, tumeshuhudia hali mbaya sana, na sasa imefikia kiwango cha kutisha.

Mlipuko huu wa sasa wa Ebola, ambao ni wa 17 kuwahi kuikumba nchi hiyo, ulitangazwa rasmi mnamo Mei 15 na umekuwa ukijikita zaidi katika mkoa wa Ituri, huku visa vingine vikiripotiwa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini.

Ugonjwa huu wa virusi, ambao mara nyingi husababisha mauti, huenea kupitia kugusana moja kwa moja na majimaji ya mwili (damu, mate, nk) kutoka kwa watu au wanyama walioambukizwa. Dalili zake kuu ni pamoja na homa kali na kutapika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *