
Costa Rica itamteua Rebeca Grynspan, mkuu wa sasa wa Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD), kwa nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, nchi hiyo ya Amerika ya Kati imetangaza Jumatano, Oktoba 8, 2025.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Waziri wa Mambo ya Nje wa Costa Rica Arnoldo André ametangaza kugombea kwa makamu wa rais wa zamani wa Costa Rica wakati wa hafla ya wanadiplomasia huko San José. Amebainisha kwamba Bi. Grynspan “mwenye ujuzi zaidi” na kwamba “kugombea kwake kutaiweka nchi kileleni.” Michelle Bachelet wa Chile pia atagombea nafasi hii.
Kama mkuu wa UNCTAD tangu mwaka 2021, Rebeca Grynspan, mwanauchumi mwenye umri wa miaka 69, amekabiliwa na changamoto kubwa kwa biashara ya kimataifa, kama vile mabadiliko ya hali ya hewa na migogoro huko Gaza na Ukraine.
Pia aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Waziri wa Nyumba, na Waziri wa Uratibu wa Masuala ya Uchumi na Kijamii. Kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka 1998, alihudumu kama Makamu wa Rais katika serikali ya Rais wa mrengo wa kati José María Figueres.
Amekuwa na taaluma ya kipekee katika Umoja wa Mataifa, akishikilia nyadhifa za juu ndani ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP). Mnamo mwaka 2010, aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, UN.