
Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan amewasili India leo Alhamisi, Oktoba 9, kwa ziara isiyokuwa ya kawaida ya siku mbili, shirika la habari la AFP limeripoti. Hii ni hatua mpya katika juhudi za serikali ya Taliban kupata kutambuliwa kimataifa, serikali ya India imetangaza.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Karibu (…) kwa Mawlawi Amir Khan Muttaqi kwa kuwasili kwake New Delhi,” ameandika msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya India Randhir Jaiswal kwenye ukurasa wake wa X. “Tunatazamia kujadiliana naye masuala ya nchi mbili na kikanda.”
Urusi ninchi ya kwanza kuitambua serikali ya Taliban nchini Afghanistan
Urusi mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu, iliitambua rasmi serikali ya Taliban nchini Afghanistan, ikiendelea na kufufua uhusiano wake wa kidiplomasia na Kabul, mashirika ya habari ya Urusi yaliripoti Julai 3. “Inatambuliwa,” Mwakilishi Maalum wa Rais wa Urusi kwa Afghanistan, Zamir Kabulov, aliambia tu shirika la habari la serikali la RIA Novosti. Habari hii ilithibitishwa na Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi kwa TASS.
Huu ni “uamuzi wa kijasiri” wa Urusi, ambayo ni nchi ya kwanza kutambua serikali ya Taliban, na “itaweka mfano kwa wengine,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan Amir Khan Muttaqi alisema wakati wa mkutano na Balozi wa Urusi huko Kabul, Dmitry Zhirnov, kulingana na matangazo ya video yaliyorushwa kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Kundi la Taliban lilirejea madarakani mwaka 2021 baada ya kupindua serikali iliyokuwa inaungwa mkono na nchi za Magharibi na kuweka toleo kali la sheria za Kiislamu kwa wakazi wa Afghanistan.