#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas, amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, kuwa faraja kwa wananchi katika kipindi hiki cha maridhiano ya kisiasa, badala ya kuendeleza au kukumbusha majeraha waliyopitia wakati wa vurugu kipindi cha uchaguzi mkuu.

Brigedia Jenerali Abbas amesema wananchi wanahitaji viongozi wanaowapa tumaini jipya, kuponya makovu ya kisiasa na kuhimiza umoja na mshikamano katika jamii.

Amesisitiza kuwa wajibu wa Madiwani ni kutatua changamoto zinazowakabili wananchi, kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha rasilimali za Halmashauri zinatumika kwa manufaa ya Umma, badala ya kujinufaisha binafsi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *