‎#HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Dalmia Mikaya, amepokea jumla ya Transfoma 30 zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.2 kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

‎Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu ya umeme katika kituo cha kusambaza umeme cha Dege, kilichopo Kata ya Somangila, DC Mikaya amesema ununuzi wa transfoma hizo ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, alilolitoa Novemba 30, 2025.

‎DC Mikaya amebainisha kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza jitihada mbalimbali za kuhakikisha wakazi wa Kigamboni wanapata huduma ya umeme ya uhakika, akitambua changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara inayowakabili wananchi wa eneo hilo.

‎Ameongeza kuwa nishati ya umeme ni nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa Taifa, kwani huchochea maendeleo ya viwanda vikubwa na vidogo, pamoja na kutoa ajira kwa wananchi kupitia sekta mbalimbali.

‎Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *