Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema maendeleo ya ujenzi Katika Kampasi ya Mloganzila ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) ni matokeo ya utekelezaji wa maagizo ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kupanua wigo wa fursa ya elimu ya juu na utafiti kwa kujenga miundombinu mipya nje ya kampasi za zamani.
Profesa Mkenda amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo, ambapo amesema mradi huo wa miaka mitano unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, unalenga kujenga uwezo wa taasisi za elimu ya juu ili kuzalisha wataalamu wabobezi, kuimarisha tafiti na kuchochea maendeleo ya sekta ya afya na uchumi kwa ujumla
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Profesa Apollinary Kamuhabwa, amesema utekelezaji wa Mradi wa HEET katika Kampasi za MUHAS Mloganzila na Kigoma unagharimu Dola za Kimarekani Milioni 45.5, ambapo dola milioni 30 zinajenga katika Kampasi ya Mloganzila, na dola milioni 15 zikitumika katika Kampasi ya Kigoma.
Ujenzi ulianza Desemba 2024 na kwa sasa majengo mengi yamefikia zaidi ya asilimia 50 ya utekelezaji, mengine asilimia ukitarajiwa kukamilika ifikapo Juni 2026.