Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Filemon Makungu amesema Mkoa wa Kigoma upo salama mbali ya kuwa mkoa huo upo karibu na Mji wa Uvira Mashariki mwa Nchi ya Kidemkrasia ya Congo.
Akizungumza katika Kipindi cha Morning Magic Magic Fm Kamanda Makungu amesema Kigoma Inapaka na Nchi Congo (DRC) Upande wa ziwa Tanganyika ambako kuna waasi wa M23 na kuripotiwa baadhi ya Matukio ya Ujambazi lakini Jeshi la polisi limehakiiisha Usalama wa Raia na wali zao ni wa Uhakika .
(Ikumbukwe M23 wameanza kujiondoa katika mji wa Uvira uliopo Mashariki ya DRC Kufuatia Makubaliano ya Doha)