‎#HABARI: ‎Mbunge wa Kundi la Vijana Kanda ya Pemba, Mhe. Zainab Abdallah, amechangia kiasi cha shilingi milioni 20.7 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miradi ya maendeleo ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) visiwani Pemba.

‎Mchango huo umetolewa katika Mkoa wa Kusini Pemba wakati wa Matembezi ya Kuadhimisha Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC),Mohamed Ali Kawaida.

‎Fedha hizo zinajumuisha shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Mkoa wa Kusini Pemba na shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuendeleza jengo la kitega uchumi la UVCCM Mkoa wa Kaskazini Pemba.

‎Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Zainab amesema mchango huo ni sehemu ya jitihada zake za kuunga mkono juhudi za vijana katika kuijenga Jumuiya na kukuza miradi ya kiuchumi inayolenga kujitegemea.


‎‎Powered by #MCHEZOSUPA

‎‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.





Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *