#HABARI: Naibu Naziri wa Nishati Mh. Salome Makamba, amewaelekeza wakandarasi wanaotekeleza miradi nchini, kuhakikisha Watanzania wazawa wanapata ajira katika miradi hiyo lengo kuu likiwa ni kupunguza changamoto mtambuka ya uhaba kwa vijana lakini itasaidia kuimarisha usalama wa miradi hiyo kwakuwa wananchi watakuwa wameshiriki katika ujenzi.
Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba, ameyasema hayo wakati akitembelea na kukagua mradi wa Upanuzi wa kituo cha kupooza Umeme cha IBADAKULI Shinyanga, unaojengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 25 za kitanzania ambapo mradi umefikia asilimia 43.
Kaimu Mkurugenzi wa usimamizi wa miradi ya TANESCO Makao makuu Mhandisi Frank Mashalo, amesema mradi huo utakapokamilika utasaidia kuimarika kwa upatikanaji wa umeme nchini, huku akiwaalika wawekezaji kuja Tanzania kuwekeza viwanda vikubwa vya kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa kuwa unmeme unapatikana wakutosha.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania