#HABARI: Wadau wa masuala ya teknolojia nchini wameiomba Serikali pamoja na wadau wa maendeleo kuyapa kipaumbele matamasha ya te…#HABARI: Wadau wa masuala ya teknolojia nchini wameiomba Serikali pamoja na wadau wa maendeleo kuyapa kipaumbele matamasha ya te…

#HABARI: Wadau wa masuala ya teknolojia nchini wameiomba Serikali pamoja na wadau wa maendeleo kuyapa kipaumbele matamasha ya teknolojia kuliko matamasha mengine, wakieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuibua bunifu zitakazotoa majibu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii katika kipindi hiki cha mageuzi makubwa ya kidijitali duniani.

Wito huo umetolewa wakati wa Tamasha la Microspace Summit 2026 lililofanyika jijini Dodoma, ambapo washiriki mbalimbali wakiwemo wabunifu wa teknolojia, wanafunzi, vijana na wataalamu wa TEHAMA walikutana kujadili nafasi ya teknolojia katika maendeleo ya taifa.

Wadau hao wamesema kuwa Tanzania ina vijana wengi wenye uwezo mkubwa wa ubunifu, lakini bado wanakosa majukwaa ya kutosha ya kuonesha na kukuza kazi zao ili ziweze kufikia soko la kitaifa na Kimataifa.

Aidha, wameeleza kuwa matamasha ya teknolojia yana mchango mkubwa katika kuchochea ubunifu, kuhamasisha matumizi ya teknolojia na kuwajengea vijana mazingira ya kujifunza, kushirikiana pamoja na kupata fursa za uwekezaji.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *