Dawati la jinsia na watoto wilaya ya Shinyanga limefanikiwa kutatua migogoro itokanayo na masuala ya ukatili wa kijinsia katika …Dawati la jinsia na watoto wilaya ya Shinyanga limefanikiwa kutatua migogoro itokanayo na masuala ya ukatili wa kijinsia katika …

Dawati la jinsia na watoto wilaya ya Shinyanga limefanikiwa kutatua migogoro itokanayo na masuala ya ukatili wa kijinsia katika manispaa ya Shinyanga hususani kesi za matunzo ya watoto ambapo wanaume wamebainika kutelekeza familia zao na kuacha kuhudumia watoto.

Mkaguzi wa jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga Jane Mwazembe amebainisha hayo wakati wa etekelezaji wa kampeni ya msaada wa kisheria mkoani Shinyanga na kueleza kuwa kampeni hiyo imerahisisha uwafikia watu wengi katika maeneo mbalimbali.

Mratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria mkoa wa Shinyanga Raulent Burilo amekiri kuwepo kwa changamoto ya ukatili kwa wanawake na watoto na kufanikiwa kutatua changamoto hizo kupitia kampeni hiyo.

Mkurugenzi msaidizi kutoka wizara ya katiba na sharia sehemu ya uzungatiaji huduma ya msaada wa Kisheria amesema kampeni hiyo pia imejikita pia katika utatuzi wa masuala ya kijinsia kiuchumi katika familia huku ikibainishwa kuwa uweepo wa wanasheria katika kampeni ya msaada wa kisheria umerahisha utatuzi wa migogoro ya ukatili wa kijinsia hususani katika kupeleka kesi hizo mahakamani.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *