#HABARI: Afisa Ardhi Mteule wa Mkoa wa Dodoma Bw#HABARI: Afisa Ardhi Mteule wa Mkoa wa Dodoma Bw

#HABARI: Afisa Ardhi Mteule wa Mkoa wa Dodoma Bw. Letare Shoo amesema kwa siku 15 za utekelezaji wa awamu ya pili ya kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia katika Mkoa wa Dodoma, Idara ya ardhi kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria imepokea jumla ya kero 887 za wananchi wenye changamoto za ardhi katika Mkoa huo, wananchi wakimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kampeni hiyo ambayo imeondoa michakato mirefu na gharama kubwa katika kutafuta suluhu mbalimbali za migogoro hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumamosi Mei 16, 2026, Bw. Shoo amebainisha kuwa kupitia mashirikiano ya Idara ya ardhi Mkoa wa Dodoma na Wizara ya Katiba na sheria, tayari pia wanashughulikia migogoro mingine 62 iliyosalia, wakidhamiria kuikamilisha kwa siku za karibuni.

Kampeni hiyo ya msaada wa kisheria ya Mama Samia imemuwezesha pia mwananchi kupata elimu mbalimbali kuhusu masuala ya ardhi ikiwemo uhamishaji wa umiliki wa vipande vya ardhi huku pia banda hilo likitoa hati za ardhi ndani ya siku moja ambapo kwa siku 15 za utekelezaji wa Kampeni hiyo Mkoani Dodoma, Jumla ya hatimiliki 130 zimetolewa kwa wananchi waliokuwa na nyaraka zote za kuthibitisha uhalali wa umiliki wa ardhi husika.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *